This post is also available in:
wezesha Sibusiso
Utabadilisha maisha ya mtoto?
Mwezeshe mtoto kupata huduma ya mazoezi tiba. Kwa mchango wako, tunaweza kuhakikisha kwamba mtoto anapokea mazoezi tiba au vifaa saidizi vinavyolingana na mahitaji yake. Hii iitasaidia mtoto kushiriki kikamilifu zaidi katika shughuli za kijamii pamoja na familia yake.
Kwa mchango wa €10 kwa mwezi, unaweza kumwezesha mtoto kupata kiti mwendo, na kwa mchango wa €30 kwa mwezi, mtoto anaweza kupata huduma ya mazoezi tiba kwa mwezi mzima. Na ikiwa ungependa kuchangia zaidi ya , €500 itatoa nafasi ya mtoto na mama yake au mlezi wake kukaa kituoni sibusiso kwa wiki nne kwa ajili ya huduma za mazoezi tiba au huduma za utengamao.Kushiriki katika mpango wa miezi sita kwa kijana hugharimu takriban €1,000. Tunathamini sana kila msaada tunaopokea. Shukrani kwa mchango wako, tunaweza kusaidia watoto wengi zaidi nchini Tanzania.
Chaguzi za kuchangia
Kuna chaguzi au njia kadhaa za kuchangia kazi za Sibusiso.
Kampeni za michango
Sibusiso nayo huendesha kampeni mara kwa mara! Je, utatusaidia?
Hadithi ya mwenzi
Rijk Zwaan imehusika kama mshirika mwaminifu katika Sibusiso tangu kuanzishwa kwake. Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya kimataifa ya ufugaji wa mbogamboga Rijk Zwaan, Helen Bos, mwenyekiti wa Tume ya Ushirikiano wa Maendeleo (COS), anaeleza kwa shauku: Rijk Zwaan ni biashara ya kweli ya familia, iliyokita mizizi katika jamii na yenye uwajibikaji wa kijamii katika DNA yake. Tunataka kuchangia kikamilifu katika usambazaji wa chakula duniani na kuongeza matumizi ya mboga kwa kuweka msingi wa mboga zenye afya na zinazovutia. Kwa COS, tunaweza kusaidia miradi (ya kimataifa). Wakati mwingine tunafanya hivi kwa kuchangia mbegu, wakati mwingine tunachangia utaalam wa kiufundi, au tunatoa msaada wa kifedha. .
” Tuna uhusiano wa karibu na Sibusiso kwa sababu sisi ni majirani wa Arusha ,” anasema Helen.Tunaweza kujionea jinsi programu ilivyofanikiwa. Tiba na lishe bora huchangia kweli ukuaji bora wa watoto wenye ulemavu wa akili. Pia tunaona kwamba watoto na wazazi wao hutembelewa majumbani mwao, na kwamba hali ya unyanya paa na kufichwa ndani kutokana na kuwa na mtoto mwenye ulemavu kunazidi kupungua zaidi kutokana na familia kuzidi kupata uelewa zaidi kuhusu ulemavu na matumaini na msaada . Tunatoa michango ya fedha mara kwa mara, kwa mfano, kuchangia wakati wa Krismasi badala ya kutoa zawadi za Krismasi kwa wafanyakazi. Tunawafahamisha wenzetu kuhusu mambo yote yanayoendelea huko Sibusiso ili waweze kuelewa athari chanya ya misaada yetu na umuhimu wa kuendelea kushirikiana katika kuleta mabadiliko katika maisha ya watoto hawa. ‘, anasema Helen Bos.